Rais Trump amteua Jaji Amy Coney Barrett katika Mahakama Kuu

Jaji Mhafidhina wa Jimbo la Indiana, Amy Coney Barrett ameteuliwa na Rais wa Marekani, Donald Trump kuchukua nafasi ya Ruth Bader Ginsburg katika Mahakama Kuu.

Baada ya uteuzi huo Barret anatarajiwa kuidhinishwa Seneti huku viashiria vya kumuidhinisha kwa wingi ukitarajiwa baada ya Kiongozi wa walio wengi kwenye Bunge la Seneti, Mitch McConnell akionyesha kufurahia uteuzi huo.

Rais wa Marekani,Donald Trump na Jaji mteule wa Mahakama Kuu,Amy Coney Barrett katika maeneo ya Ikulu ya White House mjini Washington, Marekani. (Alex Brandon/the Associated Press).

Kwa mujibu wa taratibu za Marekani,wateule wa Mahakama ya Juu ni lazima waidhinishwe kwa wingi wa kura katika Bunge la Seneti ambalo kwa sasa linadhibitiwa na Republican.

"Leo nina furaha kumteua mmoja wa watu wenye busara na mwenye kipawa cha sheria katika Mahakama Kuu.Ni mwanamke mwenye mafanikio yasiyo na kifani, akili kubwa, sifa nzuri na uaminifu thabiti kwa katiba,"amesema Rais Trump katika hafla rasmi iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington ambapo

Uteuzi huo unakuja baada ya kifo cha Jaji wa Mahakama ya Juu ya Marekani, Ruth Bader Ginsburg (87) ikiwa ni siku chache zilizopita. Marehemu Ginsburg anatajwa kuwa alikuwa ni mpiganiaji wa haki za wanawake ambaye alikuwa jaji wa pili mwanamake katika mahakama hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news