TLS:Sakata la Fatma Karume si kamati ya chama

Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili cha Tanganyika (Tanzania Bara)- Tanganyika Law Society-TLS) limesema kuwa, uamuzi wa kumuondoa katika Rejesta ya Mawakili wa Tanzania Bara, Wakili Fatma Karume, uliotolewa leo Septemba 23, 2020 ni wa Kamati ya Mawakili (Advocates Committee) kwa mamlaka yake chini ya Sheria ya Mawakili (Advocates Act Cap 141 R.E 2002 na si Kamati ya Maadili ya Chama cha Mawakili cha Tanganyika (Tanzania Bara) (The Ethics Committee of Tanganyika Law Society).
Wakili wa kujitegemea Fatma Karume (Shangazi) ambaye jina lake limeondolewa katika Rejesta ya Mawakili wa Tanzania Bara leo Septemba 23, 2020 na Kamati ya Mawakili. (Mtandao).

Hayo yamebainishwa na Rais wa TLS,Dkt.Rugemeleza Nshala kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma ambayo imeonwa na Diramakini.

Dkt. Nshala amesema kuwa, kamati hizo zina mamlaka tofauti na zimeanzishwa kwa sheria na mamlaka tofauti.

"Kamati ya Mawakili imeanzishwa na Sheria ya Mawakili (Advocates Act Cap 141 R.E 2002) wakati Kamati ya Mmaadili ya Chama cha Mawakili Tanganyika (The Ethics Committee of Tanganyika Law Society) imeanzishwa na Baraza la Uongozi la TLS kwa mamlaka yake ya kuanzisha kamati zake chini ya Sheria ya Tanganyika Law Society, Sura Namba 307 ya Sheria za Tanzania.

"Hivyo ni makosa makubwa kuwahusisha wajumbe wa Kamati ya Maadili ya TLS na uamuzi huo na kusambaza majina yao katika mitandao ya kijamii,"amefafanua Dkt.Nshala.

No comments

Powered by Blogger.