Zitto Kabwe: Nipeni miaka mitano nikakamilishe mambo muhimu

 "Ndugu zangu wana Kigoma, endpo mtanipa ridhaa ya kuwatumikia kwa kipindi cha miaka mitano naahidi kutekeleza mambo manne yaliyobaki na lengo langu ni kuipandisha Kigoma katika hadhi inayohitajika na baada ya miaka mitano kuisha mnaweza kufanya maamuzi nani mtamuweka katika nafasi hii ya ubunge;

 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo na Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Zitto  Kabwe Z.Ruyagwa ameyasema hayo Septemba 12,2020 wakati akizindua kampeni za ubunge katika jimbo hilo zilizofanyikia Kawawa ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

 Amesema, endapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo atafanyia kazi mambo manne kati ya 11 ambayo tayari yameshafanyiwa kazi ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni zake kipindi anaomba ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika miaka mitano inayoishia sasa.

Kabwe amesema, ahadi 15 alizozitoa mwaka 2015 kati ya hizo 11 zimekamilika na zilihusisha ujenzi wa barabra za ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji yenye urefu wa kilomita 15 pamoja na ujenzi wa forodha ya Ujiji.

No comments

Powered by Blogger.