Azam FC yaziacha Simba, Yanga SC kwa alama nane

Wanalambalamba Azam FC wameendeleza rekodi yake ya kushinda kila mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwanyoosha Ihefu FC kwa mabao 2-0 ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ayoub Lyanga 55' na Iddi Suleiman (Nado) 83' wote wakimalizia kazi ya Prince Dube Mpumelelo wamewezesha shangwe hiyo kwa Azam FC.

Hadi mtanange huo unamalizika Azam FC walikuwa ndiyo washindi hivyo kujikusanyika alama zote tatu ambazo zimewawezesha kufikisha alama 21 baada ya kucheza mechi saba hadi sasa.

Kwa matokeo haya ya Oktoba 20, 2020 Azam FC wanawazidi mabingwa watetezi, Simba SC na mabingwa wa kihistoria, Yanga SC kwa alama nane.

Mbali na mechi hiyo, mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imetoa sare ya 1-1 na KMC Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku Mwadui FC imeichapa Mbeya City 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 0-0 na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

No comments

Powered by Blogger.