Jubilee watishia kumng'oa Makamu wa Rais William Ruto kwa kumdharau Rais Kenyatta

Makamu wa Rais wa Kenya, William Kipchirchir Samoei Arap Ruto (William Ruto) huenda akangolewa ndani ya chama tawala cha Jubilee nchini Kenya kwa madai ya kukiuka taratibu na kuvunja maadili katika chama, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Raphael Tuju ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho amesema hayo yanaweza kufikiwa kutokana na namna ambavyo Makamu huyo amekuwa akifanya mambo kinyume na taratibu.

Tuju amemtuhumu Makamu wa Rais Ruto kwa kudai kuwa ni mtu mjeuri ambaye pia ameyapa madharau kipaumbele, hivyo kuchangia kutomuheshimu mkuu wake ambaye ni Rais Uhuru Kenyatta wa Jamhuri ya Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 2, 2020 inaeleza kuwa, chama kinasikitishwa na tabia hizo huku pia kikikemea tabia za watu wa karibu wa Makamu huyo wa Rais kutumia maneno ya kashfa na kejeli kwa viongozi waandamizi wa Serikali

Pia chama hicho kimemtuhumu, Ruto kwa kujaribu kufanya mapinduzi huku Rais Uhuru Kenyatta akiwa Ufaransa. Oktoba Mosi,2020 Ruto alijibu katika mtandao wake wa Twitter kwamba ameshangaa kwamba ziara yake ya makao makuu ya chama hicho cha Jubilee ilikuwa habari kuu.

Aidha, inaelezwa kuwa, uongozi wa chama hicho kwa sasa umesema kwamba hautamruhusu Ruto kuingia katika makao hayo pia hautamruhusu kuendesha kampeni zake za urais kutoka katika ofisi hiyo.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news