KMC FC yatuma salamu Ruvu Shooting kesho

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imejipanga kuhakikisha kwamba inakwenda kuifunga timu ya Ruvu Shooting mchezo utakaopigwa kesho saa 14.00 mchana katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,imeandaliwa na Christina Mwagala (KMC FC).
Maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kikosi hicho kipo tayari kuvaana na wapinzani hao katika soka na hivyo kuleta furaha kwa mashabiki wa timu ya KMC FC.
Katika mchezo huo timu ya KMC FC ambao ni wageni dhidi ya Ruvu Shooting imejiandaa kufanya vizuri na hivyo kurudisha hari waliyokuwa nayo wakati Ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021 ulipoanza Septemba, mwaka huu ambapo iliweza kushinda michezo mitatu mfululizo.
Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mzawa, Habibu Kondo kwa kushirikiana na mshauri wa Benchi la ufundi,John Simkoko hadi sasa hakina majeruhi na wachezaji wote wana afya nzuri.
KMC FC hadi sasa imecheza michezo sita ambapo kati ya hizo imeshinda michezo mitatu, imepoteza miwili na kutoka sare ya kutokufungana mchezo mmoja ambao ulikuwa dhidi ya Coastal Union ya mkoani Tanga na kuiwezesha kuwa na alama 10 huku ikiwa kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.

No comments

Powered by Blogger.