NEC kuwapa kipaumbele wenye mahitaji maalum Uchaguzi Mkuu Oktoba 28,2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) imewatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu kwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu, wajawazito , akina mama wanaonyonyesha ikiwemo wazee na wagonjwa watakaojitokeza kupiga kura wakati wa siku ya uchaguzi,anaripoti Anthony Ishengoma,Shinyanga.

Aidha,NEC imetoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu wa macho kwa kuweka kifaa cha maandishi ya nukta nundu kwa kila kituo cha kupigia kura kwa wale wenye uwezo wa kutumia kifaa hicho, lakini pia wale wasioweza kuambatana na mtu wanayemwamini ili kuwasaidia kupiga kura.
Baadhi ya viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika picha ya pamoja na wa watu wenye mahitaji mahalumu wakati wa Kikao cha Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga katikati ni Bi. Happy Aloys Mlemavu wa viungo.

 Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria NEC, Bw. Leonard Baraka akiongea wakati wa Kikao cha Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga leo mkoani Shinyanga.

Akiongea wakati wa Kikao cha Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga leo mkoani Shinyanga Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria NEC, Bw. Leonard Baraka ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema, tume imetoa ruhusa kwa wasiojua kusoma na kuandika waruhusiwe kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Aidha, Bw. Baraka ameongeza kuwa tume inasisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeini zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa na maneno ya uchochezi yanayotishia usalama na amani ya nchi.

 Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga wakifuatilia jambo wakati wa kikao chao na Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mkoani Shinyanga.

Wakati huo huo Afisa kutoka Tume ya Uchaguzi Bi. Nuru Riwa Kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia liongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Nchini amesema kuwa Walemavu waliojiandikisha kupiga kura ni ni takribani 13 elfu.

 Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bi.Nuru Riwa akiongea wakati wa Kikao cha Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Shinyanga leo mkoani Shinyanga.

Aidha, Kiongozi huyo wa Tume ya Taifa Uchaguzi amewataka wagombea na vyama vyao kuepuka kufanya kampeini ambazo zina viashiria vya ubaguzi katika misingi ya jinsi, ulemavu, ukabila, udini,maumbile au rangi.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Walemavu Mkoa wa Shinyanga Mzee Richard Mpongo ameomba Tume ya Uchaguzi kuwata wagombea kuweka wakalimani kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kusikia ili nao waweze kujua wagombea wao wanaongea nini wakati wa kunadi sera zao.

Naye Bi.Happy Aloys ambaye ni Mlemavu wa Viungo ametaja changamoto inayowakabili walemavu wa viungo kuwa ni kushindwa kufika katika maeneo ya kampeini lakini pia akaongeza kuwa ni hatari kwa walemavu hao endapo itatokea vurugu wakati wa mikutano ya wagombea mbalimbali wa vyama vya siasa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga katika mkutano uliowakutanisha watu wenye mahitaji maalum, viongozi wa dini, Asasi za kiraia, Wazee na baadhi ya makundi ya vijana wa Mkoa wa Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news