TAKUKURU yaokoa gari, pikipiki na Milioni 55/-

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imeokoa gari, pikipiki tatu na fedha taslimu shilingi milioni 55,561,800, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

"Leo tarehe 10, 2020 ndugu waandishi wa habari nimewaita kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mwanza kipindi cha Julai hadi Septemba 2020.

"Ndugu waandishi wa habari, TAKUKURU Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kuokoa gari moja aina ya Toyota Landcruizer lenye namba za usajili T 824 BGY, pikipiki tatu aina ya DT 125 na fedha kiasi cha shilingi milioni 55,561,800 katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2020;

Amesema, mali hizo zilizookolewa kwa maana ya gari na pikipiki zilikuwa mali za Chama cha Kutetea Maslahi ya Wakulima wa Zao la Pamba Tanzania (Tanzania Cotton Growers Association-TACOGA).

"TAGOGA ni chama kilichokuwa kinawakilisha wakulima katika kutetea maslahi yao. Hata hivyo, mnamo tarehe 23 Desemba ,2017 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika mkutano wa wadau wa pamba uliofanyika mjini Shinyanga, alitangaza rasmi kuivunja Tanzania Cotton Growers Association (TACOGA) kama mwakilishi wa wakulima wa pamba. Badala yake alisema, Serikali inafufua ushirika kupitia vyama vya msingi na kupitia mfumo huo wakulima watapata mwakilishi katika masuala yote yanayohusu.Pamoja na kuivunja TACOGA Waziri Mkuu aliagiza mali zote zilizokuwa zinamilikiwa na chama hicho zikabidhiwe kwa Bodi ya Pamba.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Bw.Emmanuel Stenga wakati alipokuwa akiongea na  waandishi wa habari ofisini kwake leo Oktoba 16, 2020.

"Naomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza waendelee kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ili tuweze kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria,"amesema Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news