Tani 5.6 za bangi zakamatwa zikipelekwa sokoni

Maafisa wa Serikali ya Morocco wametangaza kuwa, wamefanikiwa kukamata zaidi ya tani 5.6 za bangi katika operesheni mbili tofauti zilizofanyika jana karibu na mji wa Casablanca, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la MAP, askari wa Kikosi cha Gadi ya Fukwe cha Morocco, jana walifanya doria katika ufukwe wa kilomita nne Magharibi mwa mji wa al Hoceima wa Kaskazini mwa nchi hiyo na kukamata marumbesa 117 ya bangi yenye uzito wa tani nne.

MAP imeeleza kuwa,madawa hayo ya kulevya yalikuwa yamefichwa kwenye mtaro karibu na ufukwe wa Inouaren yakisubiri kusafirishwa kimagendo kwa njia ya baharini kwenda nje ya nchi. Aidha, katika opereseheni ya pili,maafisa wa kulinda usalama katika mji wa Guelmim nchini humo walifanikiwa kukamata bangi yenye uzito wa tani 1.63.
Marumbesa yaliyofungwa kwa namna yake yakiwa yamejazwa bangi kwa ajili ya kupeleka sokoni kutoka nchini Morocco.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news