Tetesi Ulaya:Manchester City imekataa dau la £15.4milioni,marupurupu kutoka Barcelona kumtoa Eric Garcia

Ipo hivi,Football Insider inaripoti kuwa, Klabu ya West Ham ipo katika mazungumzo ya kumsajili beki wa England,Craig Dawson (30) kutoka Watford. Huku Telegraph ikiripoti kuwa,Barcelona imepoteza zaidi ya £181m kama mapato kutokana na mlipuko wa virusi vya corona (Covid-19).

Nayo Star inaeleza kuwa, beki wa Manchester City na England, John Stones (26) alikataa mbadala wa kuondoka kwa mkopo kuelekea Totenham kutokana na masuala ya kifamilia.

Sky sports inaripoti kuwa, Porto ina shauku ya kumpa kandarasi mchezaji wa West Ham na Brazil Felipe Anderson (27) kwa mkopo.

Eric Garcia.(Onefootball).

Wakati huo huo,Manchester City imekataa dau la £15.4milioni na marupurupu kutoka kwa klabu ya Barcelona kumnunua beki wa Uhispania Eric Garcia (19) katika dirisha dogo. Kwa upande wa Goal inaripoti kuwa,
Liverpool ilipokea maombi ya winga wa Switzerland Xherdan Shaqiri (28).

Ni wakati wa dirisha la uhamisho na wanatarajia atabaki katika klabu hiyo hadi mwezi Januari,mwakani kwa sababu hawako tayari kumuuza kwa mkopo kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments