Tetesi:Kylian Mbappe anaweza kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo Juventus

Kwa mujibu wa Express, Klabu ya Arsenal inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mlinzi wa Villarreal, Pau Torres (23) kwa kitita cha £35milioni mwezi Januari, mwakani huku Football Insider ikiripoti kuwa Klabu ya Cardiff City imekubali kumsajili winga wa Liverpool, Harry Wilson (23) kwa mkopo.

Wakati huo huo, vilabu vya Derby County na Nottingham Forest vinatajwa kumwania mchezaji huyo wakiamini ana nafasi kubwa. Sky Sports inaripoti kuwa, Klabu ya Middlesbrough inajaribu kukamilisha usajili wa winga Yannick Bolasie (31) kwa mkopo kutoka Klabu ya Everton.

Katika hatua nyingine, Sky Sports inaripoti kuwa, Klabu ya Chelsea walikuwa tayari kumlipa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi (33) mshahara wa £1milioni kwa wiki kwa uhamisho wenye thamani ya £225milioni.

Metro inaripoti kuwa, kiungo wa Manchester United, Bruno Fernandes (26) amekataa kumnyooshea kidole Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wenzake baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Klabu ya Tottenham kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za Kimataifa.

Cristiano ronaldo and Kylian Mbappe. (Getty Images).

Wakati huo huo, Klabu ya Juventus wanapanga uhamisho wa £360m kumnasa mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe (21) ambapo kwa mujibu wa Mirror, klabu hiyo ya Serie A inaweza kumpeleka Cristiano Ronaldo (35) upande wa pili.

Kwa mujibu wa Mail, Klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund haina mpango wa kumuuza winga wa England Jadon Sancho (21) katika dirisha dogo la usajili la Januari,mwakani ambaye alihusishwa na Manchester United katika majira ya joto.

No comments

Powered by Blogger.