Tullow yaingia makubaliano na Total uchimbaji mafuta Uganda

Serikali ya Uganda imeipa ruhusa kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow ya kuuza mgao wake wa machimbo ya mafuta katika eneo la Ziwa Albert kwa Kampuni ya Ufaransa ya Total, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Lengo ni kutoa fursa ya kuanza kwa hatua ya mwisho ya uwekezaji katika kuchimba na kusafirisha mafuta ya Uganda kwa soko la Kimataifa.

Sambamba na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hayo kutoka mjini Hoima, Uganda hadi jijini Tanga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kampuni ya Tullow kupitia taarifa kwa umma imeeleza kwamba, Serikali ya Uganda na Mamlaka ya Kukusanya Kodi Uganda (URA), zimefikia makubaliano kuhusu namna ya kulipa ushuru kutokakana na kuuza kwa vifaa vyake kwa Kampuni ya Total.

“Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda ameidhinisha hatua ya kupeana vifaa na mali za Tullow kwa Kampuni ya Total pamoja na idhini ya utendaji kazi katika machimbo namba mbili.Kwa sababu masharti yote ya serikali yametimizwa, Tullow inatarajia kumaliza shughuli zake katika muda wa siku chache zijazo na kupokeza idhini ya kufanya kazi kwa Total,”imefafanua sehemu ya taarifa hiyo ya Tullow.

Kampuni ya Tullow itapokea dola milioni 500 katika hatua ya kwanza na dola milioni 75 pale ambapo maamuzi ya uwekezaji ya mwisho yatakapochukuliwa kuhusu mradi huo wa kuchimba mafuta. Kampuni ya Tullow pia ina haki ya kupokea sehemu ya fedha zitakazopatikana katika awamu ya kwanza ya uchimbaji mafuta hayo nchini humo.

Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa za kisheria, kuhusiana na uchimbaji mafuta yake yanayotarajiwa kuileteaa dola bilioni 3.5 za Kimarekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news