Watanzania milioni 29 wajiandikisha kupiga kura vituo elfu 80

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema hadi sasa wananchi waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 29,188,347 huku vituo nchi nzima vikiwa ni 80,155, kila kituo kinatarajiwa kuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

''Tofauti na chaguzi zote zilizowahi kufanyika uchaguzi huu, unagharamiwa na fedha zetu za ndani kutoka hazina na hakuna fedha yeyote iliyotolewa na wahisani,"ameeleza Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dkt.Wilson Mahera Charles.

Ameongeza kuwa, ''Zanzibar kampeni zitahitimishwa Oktoba 26, ili kupisha uchaguzi wa awali kwa urais, wabunge na madiwani, ambao utafanyika Oktoba 27, ambayo kwa Tanzania bara ndiyo siku ya mwisho kufanya kampeni.

“Jumla ya asasi za ndani 97 zimepewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura na mpaka sasa jumla ya taasisi 17 kutoka nje zimepewa vibali kwa ajili ya kufanya uangalizi katika uchaguzi mkuu,”Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera Charles ameongeza.

No comments

Powered by Blogger.