Watendaji Sekta ya Ardhi waaswa kufanya kazi kwa ushirikiano

Watendaji wa Sekta ya Ardhi katika Halmashauri ya Manyoni mkoani Singida, wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi zaidi, anaripoti Eliafile Solla.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Singida, Bw. Speratus Ruteganya, katika kampeni maalum iliyozinduliwa na wizara ya siku ya elimu ya mlipa kodi ambayo hutekelezwa kila siku ya Ijumaa.
Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi makao makuu Dodoma wakipeana maagizo namna ya kutekeleza zoezi la elimu ya mlipa kodi nje ya Ofisi ya Halmashauri ya Manyoni, kabla ya kuanza utekelezaji wa zoezi hilo nyumba kwa nyumba katika mtaa wa Majengo. (ARDHI).

Akizungumza na kikosi kazi maalum kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kilichofika wilayani Manyoni kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu kodi ya pango la ardhi, Ruteganya alisema umoja na ushirikiano ndiyo nguzo pekee ya kufikia malengo katika sekta ya ardhi.

Aliongeza kwamba, wananchi wanachohitaji ni elimu tu kwani wakielimika kodi itapatikana pamoja na taarifa muhimu za umiliki.

Kwa upande wake kiongozi wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Bw.Adam Komba alisema, lengo la Wizara kuanzisha siku ya elimu kwa mlipa kodi ni kuhakikisha wananchi wanapewa elimu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuboresha taarifa zao za umiliki.

Baadhi ya mafisa kutoka makao makuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakigawana ramani za upimaji (survey plan) za mtaa wa Majengo katika Halmashauri ya Manyoni kabla ya kuanza kupita nyumba hadi nyumba kutoa elimu kuhusu kodi ya pango la ardhi. (ARDHI).

Alisisitiza kwamba, kutokana na mabadiliko ya teknolojia hasa kwenye utoaji wa huduma, wizara ina mpango wa kuboresha mifumo yake ya utoaji huduma hivyo pamoja na kutoa elimu kuhusu kodi ya pango la ardhi pia zoezi linalenga upatikanaji wa taarifa muhimu za kila mmiliki wa kipande cha ardhi.

Naye afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya Manyoni, Bi. Zamzam Seif, aliishukuru Wizara ya Ardhi kwa hatua mathubuti iliyochukua ya kuboresha taarifa za wamiliki Ardhi na pia kampeni ya siku ya elimu ya mlipa kodi. Zam zam alisema, kitendo cha Wizara kutuma kikosi kazi Wilayani hapo na kimewapa moyo sana na nguvu mpya ya kufanya kazi.

Siku ya elimu ya Mlipa kodi ni kampeni maalum iliyoanzishwa na Wizara ya Ardhi ambapo, kila siku ya Ijumaa kikosi kazi kitakuwa kinapita mitaani kutoa elimu nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wamiliki wa Ardhi wanajua sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayoisimamia sekta ya Ardhi.

Wataalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakikagua ramani za upimaji za mtaa wa Majengo wilayani Manyoni kabla ya kuanza kupita nyumba hadi nyumba kuelimisha wananchi umuhimu na jinsi ya kulipa kodi ya pango la ardhi. (ARDHI). 

Pamoja na hayo, pia lengo ni kuhakikisha Wizara inajenga ukaribu zaidi na wamiliki wa Ardhi na kuona namna bora ya kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya Ardhi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Naomba kuwasilisha maoni ya idara ya Ardhi kama mwanachi """"
    Tanzania haiwezekani tuwe na sheria zilizotungwa halafu baadhi ya watumishi
    wanazifumbia macho na hazitekelezwi ili nchi ipige hatua mfano idara ardhi
    hapa nchini imejikita kupanga maeneo na kupima tu lakini zoezi mikakati ya
    kuandaa hati miliki za wananchi haziandaliwi kama kama jinsi idara za
    upimaji na mipango miji walivyo haraka up itafikia mahala tunakuwa na namba
    za viwanja tu bila hati miliki.

    Regards,
    NGUSA charles juda | ngusaeliz@gmail.com

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news