Rais Magufuli amteua Polepole, Lulida kuwa wabunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo Novemba 29, 2020 amefanya uteuzi wa wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Chamwino jijini Dodoma, Gerson Msigwa kwanza, RaisMagufuli amemteua, Bw. Humphrey Polepole kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Humphrey Polepole ni Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pili, Rais Magufuli amemteua Bi. Riziki Said Lulida kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wabunge Wateule hao wataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.