Aliyewahi kuwa Waziri, Balozi wa Tanzania Dkt.Ng'wandu afariki

Mbunge wa zamani wa jimbo la Maswa ambaye amewahi kuwa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia na pia Balozi was Tanzania nchini Japan, Dkt. Pius Ng'wandu amefariki dunia, anaripoti Mwandishi Diramakini.Taarifa zimesema, Dkt. Ng'gwandu amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi mkoani Simiyu ambako alipelekwa haraka baada ya kupata matatizo ya shinikizo la damu.

Dkt. Pius Yasebasi Ng’wandu aliwahi kuwa Balozi wa Japan kati ya mwaka 1990 hadi 1993, Waziri wa Sayansi na Teknologia mwaka 2000 hadi 2008.

Hivi karibuni,Dkt.Ng'wandu mwenye umri zaidi ya miaka 70 alivuma mitandaoni baada ya kufunga ndoa na binti mwenye umri mdogo zaidi kuliko yeye ambapo baadhi ya watu walidai kuwa ana umri wa mjukuu wake. 

Uongozi wa Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa www.diramakini.co.tz unawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo Watanzania wote kwa kuondokewa na Mheshimiwa Dkt.Ng'wandu, Mwenyenzi Mungu amlaze mahali pema.

No comments

Powered by Blogger.