Arsenal yaitandika Chelsea 3-1

Desemba 26, 2020 ambayo ni Siku ya Kufungua Maboksi ya zawadi imekuwa ya faraja kwa mashabiki wa Klabu ya Arsenal baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mtanange huo wa Ligi Kuu ya England ambao umepigwa katika dimba la Emirates Stadium umewafanya mashabiki hao kutembea kifua mbele ikiwa walikosa ushindi kwa muda mrefu baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Manchester United. 

Mabao ya Arsenal inayonolewa na Mikel Arteta yamefungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 34 kwa mkwaju wa penalti, Granit Xhaka dakika ya 44 na Bukayo Saka dakika ya 56.

Aidha, kwa Chelsea inayonolewa na Kocha Mkuu, Frank Lampard bao lilifungwa na Tammy Abraham dakika ya 85.

Post a Comment

0 Comments