Arsenal yakiri ipo katika vita kali

Mikel Arteta ambaye ni kocha wa Klabu ya Arsenal amesema wapo katika vita vikali na wachezaji wake kwa sasa wanaumiza zaidi baada ya kupokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Everton, anaripoti Mwandishi Diramakini.
(Picha na AP).

Kichapo hicho walikipata Desemba 19, 2020 katika dimba la Goodison Park, hali ambayo imewafanya mashabiki wengi wa klabu hiyo kuendelea kujihisi wapweke.

Rob Holding wa Everton ndani ya dakika 22 alipachika bao la kwanza baadaye Arsenal kupitia Nicolas Pe'pe' ndani ya dakika 35 akasawazisha huku Everton kupitia Yerry Mina ndani ya dakika 45 akafunga hesabu ya bao la pili.

Matokeo hayo mabovu yanakuwa mara ya nane kwa Arsenal kushindwa kutokana na mechi 14 za hadi kufikia sasa katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu. 

Wakati wao wanauzunika,kocha Carlo Ancelotti wa Everton anasherehekea vyema maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuinoa klabu hiyo kwa kutinga nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

No comments

Powered by Blogger.