Balozi Kairuki atoa wito maalum kwa China kuhusu Afrika

Mjadala wa Mabalozi, Wanazuoni na wafanyabiashara umefanyika leo jijini Beijing,China kuzungumzia Mpango wa 14 wa Maendeleo wa China na fursa za ushirikiano na mataifa ya Nje, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini (Beijing).

Katika mkutano huo ambao pia Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki ameshiriki wamejadili pia fursa za uchumi katika Eneo la Soko Huru la Afrika (AfCFTA).

Katika mkutano huo Balozi Kairuki ametoa wito kwa China na Afrika kushirikiana kuongeza tija katika sekta ya kilimo kuongeza uzalishaji wa malighafi za kutosheleza mahitaji ya soko la ndani na nje.
Pia Balozi Kairuki amehimiza uwekezaji katika kuongeza thamani ya malighafi ili kuweza kuzalisha bidhaa zitakazouzwa Barani Afrika na nje ya nchi. Bila kufanya hivyo, mpango wa Soko Huru la Afrika hautakuwa na manufaa.

Post a Comment

0 Comments