Bodi mpya ya MCT yakutana, waandaa mkakati wa kuvinusuru vyombo vya habari

Bodi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imeliagiza Baraza hilo kuchukua hatua mahsusi kukutana na wadau wote wa habari kwa lengo la kuboresha hali ya uchumi ya vyombo vya habari nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Katibu wa Bodi hiyo ambaye ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema baada ya kikao cha Bodi kilichofanyika Desemba 21, 2020 kuwa hali ya uchumi ya vyombo vya habari ni mbaya na Bodi imeagiza Baraza kukutana na wadau wakiwemo wahariri, watendaji wa vyombo vya habari na wamiliki kuangalia aina bora za kufanya biashara hiyo.

“Ni muhimu tukaondokana na utaratibu wa kutegemea matangazo na mauzo kwa njia za kawaida,"amesema Mukajanga.

Bodi hiyo ya MCT ilikutana katika kikao chake cha kwanza baada ya kuchaguliwa katika Mkutano Mkuu wa MCT uliofanyika Tanga Septemba 28,2020.

Bodi hiyo ilikutana chini ya uenyekiti wa Rais mpya wa MCT Jaji Mstaafu, Juxon Mlay.

Pamoja na kujadili hali mbaya ya uchumi inayovikabili vyombo vya habari, Bodi hiyo ilijadili mpango kazi wa Baraza kwa mwaka 2021, ilipokea ripoti ya kamati ya fedha na utawala na pia ilipokea ripoti ya kamati ya maadili ya mwaka 2020 kuhusu hali ya vyombo vya habari na uhuru wa habari.

Kutokana na hali mbaya ya kiuchumu baadhi ya vyombo vya habari vimesimamisha kufanya kazi hiyo na vingine vimeamua kuendesha shughuli zao kwa mtandao.

Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa njia zote mbadala ni ngumu kwa biashara ya habari.

Bodi pia imehimiza Baraza kuendelea kukutana na serikali kwa lengo la kuboresha maendeleo ya vyombo vya habari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news