Kocha wa Manchester United ajiandaa kuleta mataji

Ole Gunnar Solskjaer (47) amesema ana matumaini kikosi chake cha Manchester United kitaiamarika zaidi na kurejea kuwa miongoni mwa watetezi wa mataji katika soka la Ulaya ikiwemo Uingereza, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kocha huyo raia wa Norway ambaye anatimiza miaka miwili ya kuinoa klabu hiyo anesema ubongo wake unafanya kazi muda wote akiwa katika dimba la Old Trafford ili kuhakikisha klabu hiyo inang'ara zaidi.

Amesema, msimu wa 2019-2020 walitinga nusu fainali za mapambano matatu muhimu na wakaingia katika katika nne bora katika Msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, hiyo ikiwa ni ishara kwamba wapo imara na watafanya makubwa zaidi.

Klabu hiyo inavaana na Leeds United, huku kocha huyo akisema yaliyopita si kipaumbele bali kwa sasa wanaangazia matokeo zaidi kwa ajili ya kusonga mbele.

No comments

Powered by Blogger.