Rose Manfere ndiye Miss Tanzania 2020-2021

 Matangazo mubashara kutoka katika Jiji la 
Biashara la Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Rose Manfere mwenye umri wa miaka 21 ametangazwa kutwaa taji la Miss Tanzania usiku wa kuamkia leo Desemba 6, 2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Aidha, nafasi ya pili imenyakuliwa na mrembo, Juliana Rwehimiza na nafasi ya tatu akiibeba Prisca Lyimo.

Kutokana na ushindi huo, Rose amezawadiwa gari aina ya Toyota Subaru Impreza toleo la Mwaka 2011 lenye thamani ya shilingi milioni 13.

Wakati mshindi wa pili Juliana ataondoka na seti ya sofa na meza ndogo ya sebuleni.

Mashindano hayo yaliyoanza saa 4:00 usiku, yalihitimishwa saa 8 usiku na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson (MB).


Post a Comment

0 Comments