Rais Magufuli ateua Manaibu Waziri 23 leo Desemba 5, 2020

Leo Desemba 5, 2020 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John W. H. Kijazi ametangaza Baraza la Mawaziri baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Balozi Kijazi akitangaza Baraza la Mawaziri hao leo Ikulu, Chamwino jijini Dodoma amesema, Rais Dkt.Magufuli amewateua wafuatao kuwa manaibu waziri akiwemo;

1:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kigahe Exaud Silaoneka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

2:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Angelina Sylvester Lubala Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

3:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Patrobas Paschal Katambi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira).

4:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Khamis Hamza Khamis kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

5:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwanaidi Ali Khamis kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango.

6:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Kipanga Juma Omary kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

7:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Festo Stephen Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI).

8:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Byabato Stephen Lujwahuka kuwa Naibu Waziri wa Nishati.

9:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. John Deogratius Ndejembi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

10:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

11:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Pauline Philipo Gekul kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

12:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ndulane Francis Kumba kuwa Naibu Waziri wa Madini.

13:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Msongwe Godfrey Kasekenya kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

14:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Ummy Hamis Nderinanga kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu).

15:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mhandisi Marryprisca Winfred Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Maji.

16:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Abdallah Hamis Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

17:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

18:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. William Tate Ole Nasha kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

19:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Marry Francis Masanja kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

20:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. David Ernest Silinde kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI).

21:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

22:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

23:Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Geophrey Mizengo Pinda kuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Wateule wote kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa wataapishwa wiki ijayo jijini Dodoma kwa tarehe na muda utakaotangazwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news