Mtuhumiwa mauaji ya askari arejeshwa mahabusu

Mahakama ya Mkoa Chake Chake Kisiwani Pemba, Zanzibar imempeleka mahabusu kwa muda wa wiki mbili mtuhumiwa, Issue Foum Machano (55) anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji aliyekuwa askari wa vikosi vya SMZ, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Luciano Makoye, mwendesha mashaka wa serikali Juma Ali Juma ameieleza Mahakama kwamba, mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo Septemba 28, 2020 majira ya saa 2 usiku.

Amesema, siku ya tukio huko Ngwachani MkoĆ ni,mtuhumiwa inadaiwa alimuua askari huyo Khalfan Juned Mohammed jambo ambalo ni kosa kisheria.

Amesema kuwa, kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 179 na 180 cha Sheria ya Adhabu namba 6 ya mwaka 2018 sheria za serikali ya Zanzibar.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu lolote kwani mahakama hiyo haina uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za aina hiyo. Kesi hiyo imepangwa kusikiliza Desemba 15, 2020 katika Mahakama ya Juu Pemba, Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments