Mwaka 2020 ulivyoacha makovu, fursa na vilio kwa Wamarekani

Mwaka 2020 utakumbukwa kama mwaka ambao Marekani iliongoza na watu zaidi walioambukizwa pamoja na kufariki duniani kutokana na virusi vya corona. 

Huu ulikuwa pia mwaka wa ufanisi kwa makampuni ya teknohama. Huu ni mwaka pia ambapo uchaguzi wa rais ulizusha utata kuwahi kushuhudiwa pamoja na ghasia na maandamano ya kupigania haki za kiraia, na kupinga ubaguzi, yalifanyika kote nchini. 

Kwa mujibu wa VOA, wachambuzi wa mambo wanasema kwamba Marekani imekuwa nchi iliyokumbwa vibaya sana na ugonjwa huo wa hatari wa corona kutokana na kutojitayarisha. 

Lawrence Gostin wa Chuo Kikuu cha George Town anasema, makosa yalianza pale mjii ilipokuwa inafunga shughuli zake zote huko China na Ulaya, Marekani ilikuwa bado haijachukuwa hatua. 

Gostin anaeleza, "Hatuja jitayarisha tulijua hali hii inatufikia ilitubidi kujitayarsha ilipofika mara ya kwanza na tatizo kubwa lililojitokeza ni upimaji. 

Mbali na tatizo hilo wachambuzi wanasema ilikuwa suala la uongozi. Rais Donald Trump hakulipatia umuhimu unaostahili tatizo hilo hata baada ya kutangazwa kuwa ni janga la afya kimataifa. 
Rais Donald Trump.

Rais Donald Trump alieleza taifa kuwa, "Kutokana na kila kitu tulichokifanya, hatari ni ndogo kwa Wamarekani kuathirika kwani tuna wataalamu mahiri kuliko mahala pengine popote duniani, tuna uwezo mkubwa wa kukabiliana na janga hilo. 

Na kufikia wakati huu tunapot ayarisha makala haya Marekani imekuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 18 na zaidi ya 340,000 wamefarki. 

Habari nzuri hata hivyo inayoleta matumaini baada ya kipindi hichi cha kipekee duniani ni kupatikana kwa chanjo na kampeni za kuwachanja watu kuanza mara moja mapema mwezi wa Disemba. 

Rais mteule Joe Biden ameweka suala hilo kuwa kipaumbele chake na kuteua mara moja tume maalum ya wataalamu kuongoza juhudi za kutokomeza ugonjwa huo. 
Rais mteule Joe Biden 

Biden, alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa Novemba mwaka huu akimshinda Rais Donald Trump kwa zaidi ya kura milioni 7 na kupata kura 306 za wajumbe wa uchaguzi. 

Matokeo hayo hayakumridhisha Rais Trump aliyeandaa kampeni ya kufikisha malalamiko mahakamani. Alifikisha zaidi ya mashtaka 50 lakini hatimae mahakama kuu ikamua kwamba hakukuwa na msingi wa mashtaka kutokana na ukosefu wa ushahidi. 

Trump hadi hivi sasa hajakubali kuwa ameshindwa na anaendelea na madai kwamba kulikuwa na wizi kwenye uchaguzi. 

Biden ataapishwa rasmi hapo Januari 20, akiwa ameweka historia mpya hapa Marekani kwa kuteua baraza la mawaizri lenye mchanganyiko wa watu na hasa kuteua wanawake wengi zaidi katika nafasi za juu kuwahi kushuhudiwa hapa nchini. 

Pia tukio ambalo haliwezi kusahaulika mwaka 2020 ni maandamano ya miezi kadhaa ya kupinga ubaguzi wa rangi na kutetea haki za kiraia kufuatia kuuliwa kwa Marekani mweusi Geoge Floyd huko Minniapolis.
George Floyd, ambaye baadae alifariki akiwa anashikiliwa na polisi, akizungumza na afisa wa zamani wa polisi wa Minneapolis Thomas Lane wakati alipokamatwa.

Tukio hilo lilionekana kwenye video pale polisi Mzungu akimwekea goti kwenye shingo lake hadi kufariki. 

Ghasia zilizuka pembe zote za Marekani na maandamano makubwa kufanyika katika mataifa mengi ya dunia. 

Maandamano hayo wataalamu wanasema huenda ndio yaliwahamasisha Wamarekani wengi zaidi kujitokeza kupiga kura kuliko wakati mwngine ule. 

Maandamano mengine makubwa yaliyofanyika ni kuadhimisha miaka minne tangu maandamano makubwa ya kudai haki za wanawake kufanika Marekani mwanzoni mwa mhula wa Rais Trump. 
Maandamano ya kudai haki za wanawake Marekani mjini Washington, DC. 

Katika utawala wake Trump ameondoa sheria kadhaa zilizopitishwa na utawala wa Barack Obama zilizokuwa zinalinda haki za wanawake kama vile kupata mishahara sawa na wanaume, kudhibiti unyanyasaji wa wanawake kingono kazini na kuondoa msaada wa serikali kwa mashirika yanayounga mkono utoaji mimba. 

Sarah Fliesch Fink wa taasisi ya kitaifa ya ushirikiano kati ya wanawake na familia wanasema, kazi kubwa kwa Biden hivi sasa ni kurudisha tena sheria na sera hizo. 

Fink anaeleza, "Kuna haja kubwa kwa utawala wa Biden na Harris na idara zote kutafakari yale yanayo hitajika kuchukuliwa hatua mapema na yale yanayohitajika kuondolewa, na yale yanayo hitaji kurudishwa. Na kwa hivyo ni muhimu kwa mambo hayo kuwekwa kwenye vipaumbele vya sera zao. 

Makampuni ya teknohama yamefaidika sana kutokana na janga la covid-19, lakini wakati huo wakubuni njia chungu nzima za mawasiliano kutokana na watu kulazimika kubaki nyumbani na kufanya kazi pamoja na wanafunzi kusoma kutoka nyumbani pia. 

Eric Ries mwandishi wa kitabu cha “The Lean Startup” anasema, teknolojia mwaka huu imeokoa maisha ya watu wengi sana. 

Eric Ries mwandishi wa kitabu The Lean Startup anasema, "Hakuna shaka hata kidogo kwa mamilioni ya watu, teknolojia imekuwa kitu cha kuokoa maisha yao. Je nani aliweza kufikiria manzoni mwa janga hili mapema mwaka huu tungeliweza kuwa na chanjo ifikapo mwisho wa mwaka. Na, je, nani alifikiria tutakuwa na apps chungu nzima za kufanya mambo mbali mbali kukidhi mahitaji yetu.
Jinsi teknolojia inavyowasaida watu kwa mawasiliano ya kikazi wakati huu wa COVID-19.

Kutokana na teknolojia hiyo wasanii hasa wanamuziki wameweza kufurahisha na kutumbuiza watu kupitia ukurasa wa mtandao kama Zoom na mengineo na mikutano takriban yote imekua ikifanyika kupitia mawasliano ya mtandao. 

Lakini pigo kubwa Marekani pia ni watu kupoteza ajira zao karibu watu milioni 30 wamepoteza ajira na biashara nyingi kubwa kubwa kufungwa. 

Kiwango cha umaskini pia kimeongezeka kufikia asilimia 19 ya Wamarekani wote kulingana na taasisi ya Pew. 

Tumeshuhudia maelfu na maelfu ya watu katika miji mbali mbali wakisubiri kupokea chakula kutoka wahisani, ikiwa ni kanisa misikiti au mashirika ya hisani mnamo kipindi hichi chote cha janga la corona. 
Kobe Bryant.

Na kwa kumaliza habari ya kusikitisha zaidi mwaka 2020 ni kifo cha mchezaji mashuhuri wa mpira wa vikapu Kobe Bryant aliyefariki kutokana na hali ya helikopta mwezi Januari.
Hayati Ruth Bader Ginsberg.  

Watu wengine mashuhuri waliofariki ni pamoja na jaji wa mahakama kuu, Ruth Bader Ginsberg, na mwanasiasa mtetezi wa haki za kiraia, John Lewis nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news