NMB yaunga mkono mapambano dhidi ya VVU

Katika kuunga mkono jitihada za udhibiti wa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini, Desemba Mosi ikiwa Siku ya Ukimwi Duniani, Benki ya NMB imetoa msaada wa fulana zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho hayo ambayo yalifanyika Kitaifa mjini Moshi, Kilimanjaro na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kukata bima ya afya.
Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela, PrayGod Godwin akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Anna Mghwira ofisini kwake msaada wa fulana zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko (kushoto) akizungumza na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (aliyepo katikati), Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela, PrayGod Godwin na Meneja Mwandamizi Huduma za Serikali, Christabel Hiza baada ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Stella Msofe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano Biashara na Serikali wa Benki ya NMB, Mkunde Joseph alipotembelea Banda la benki hiyo kwenye maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam Desemba 1, 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news