Polisi washikilia watuhumiwa 683 kwa uhalifu Tabora

Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 683 wa makosa mbalimbali Mkoani Tabora katika Oporesheni ilichukua wiki tatu katika Wilaya zote za Mkoa huo, anaripoti Tiganya Vincent.
Mkuu wa Opereshemi Maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Mwandamizi wa Jeshi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela akiwaonyesha waandishi wa Habari mjini Tabora mmoja ya mfano wa sare ya polisi waliyoikamata katika oporesheni ya wiki tatu waliyoiendesha katika Wilaya zote na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 683 wa makosa mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Opereshemi Maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Mwandamizi wa Jeshi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tabora. 

Amesema, miongoni mwa watuhumiwa hao ni 277 wamefikishwa Mahakamani na kuhukumiwa , watuhumiwa 255 bado kesi zao zinaendelea na watuhimiwa 42 wako katika uangalizi wa Polisi baada ya kutokuwepo kwa ushahidi madhubuti. 

SACP Msikhela alisema baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa ni silaha aina ya gobore moja, mapanga tisa, meno ya tembo mawili, pikipiki 34 , magodoro 10 na simu za mkononi nne. 
Mkuu wa Opereshemi Maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Mwandamizi wa Jeshi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela akiwaonyesha magodoro na vitu mbalimbali kwa waandishi wa Habari mjini Tabora walivyokamata katika oporesheni ya wiki tatu waliyoiendesha katika Wilaya zote na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 683 wa makosa mbalimbali. 

Vitu vingine vilivyokutwa kwa watuhimiwa ni vyuma vya reli viwili,runinga za aina mbalimbali 19, mfano wa sare za majeshi mbalimbali ya ndani na nje na pombe haramu ya gongo lita 408. 

Ameongeza kuwa, miongoni mwa watuhumiwa hao wamefanikiwa kukamata raia wa nje kabila Mhutu akiwa na aina mbalimbali za mfano wa are za Polisi na majeshi mengine. 

SACP Msikhela amesema, mtuhumiwa huyo akikamatwa baada ya Askari Polisi kumuona amevaa sare ambazo zinafanana na za Polisi lakini mshono wake ni tofauti. 

Amesema, baada ya kupekua begi alililokuwa amebeba ndipo walikuta sare zinazotaka kufanana na zile za Jeshi la Wananchi na nyingine zinafana na za Majeshi ya Nje. 

SACP Msikhela amesema, katika operesheni hiyo ya kuanzia tarehe 7 mwezi huu wamebaini kuwa magenge yanayojihusisha ni uvunjaji, uporaji, na wizi ni vijana ambao umri wao ni kuanzia miaka 15 hadi 21. 

Amesisitiza Jeshi la Polisi litaendelea kufanya opresheni na misako ya mara kwa mara kwa kushirikiana na raia wema ili kukomesha uhalifu mkoani Tabora

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news