Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 61(1) cha Katiba ya Zanzibar mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa kama ifuatavyo:-

1.     Bibi Salama Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

2.     Bwana Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

3.     Bwana Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

4.     Bwana Idrisa Kitwana Mustafa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi.

5.     Bwana Matar Zahor Masoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt.Abdulhamid Y.Mzee, uteuzi huo umeanza Desemba Mosi, 2020.