Rais Magufuli akagua maendeleo ya ujenzi wa Ikulu jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Desemba 8, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Ikulu jijini Dodoma na kuelezea kuridhishwa na kiwango na kasi ya ujenzi wa majengo ya ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ujenzi wa ofisi hizo ulioanza Februari 17, 2020 unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo na unafanywa kwa usanifu na muonekano sawa na Ofisi za Ikulu zilizopo jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi Luteni Kanali George William Nyisa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya ofisi mpya za Ikulu Chamwino, Dodoma Desemba 8, 2020Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu mbali mbali wakati akikagua ujenzi wamajengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.

Msimamizi wa ujenzi wa ofisi hizo, Luteni Kanali George William Nyisa amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu mbalimbali wakati akikagua ujenzi wamajengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia mafundi wa kiraia wakati akikagua ujenzi wa majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.

Akikagua majengo yanayojengwa, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na uimara wa nguzo na kuta zinazojengwa na amesema ni fahari kubwa kwa Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi badala ya kutumia wakandarasi kutoka nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wajenzi wa kijeshi baada ya kukagua majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wajenzi wa kijeshi baada ya kukagua majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mmoja wa askari wajenzi walati akikagua majengo ya ofisi za Ikulu Chamwino, Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki ujenzi huo ambapo amekumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa katika JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa ofisi za Ikulu.

Pamoja na kuwapongeza vijana hao, Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza vijana wa kiraia wanaoshiriki katika ujenzi huo ambao ni mafundi, na amewaahidi kuwa atawaangalia mara baada ya kumaliza kazi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news