Serikali yateketeza mchele tani 112 uliokuwa umefikia mwisho

Zaidi ya tani 112 za mchele wa Basmati zimeteketezwa na Mamlaka ya Udhibiti na Usalama wa Dawa na Chakula Zanzibar (ZFDA), baada ya kukamatwa katika ghala la Akhtar Enterprises (Simba Chai) lililopo Mombasa nje kidogo ya jiji la Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Tani hizo zimeteketezwa katika dampo la Kibele Wilaya ya Kati mjini Unguja baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa umefikia ukomo wa matumizi kwa binadamu

Mkurugenzi wa ZFDA, Dkt Khamis Ali Omar ameyabainisha hayo jijini hapa wakati akitoa maelezo kuhusiana na kuteketezwa kwa mchele huo.

Dkt.Omar amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kugundulika kuwa mmiliki wa ghala hilo anatoa mchele kwenye vifungashio vilivyomaliza muda wake tangu mwaka 2019 na kungiza katika vifungashio vipya ambapo utatumika mpaka 2022 jambo ambalo linahatarisha afya za walaji.

‘’Tunasikitishwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu katika kuzibadilisha bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi na kuziingiza katika vifungashio vipya bila kujali afya ya watumiaji,’’amesema Dkt.Omar.

Pia amesema, ndani ya ghala hilo wamegundua tambi ambazo zilishapitwa na wakati pamoja na mifuko mitupu ilivyobadilishwa mwaka kwa ajili ya kuzifunga upya ili kuanza kusambaza katika maduka mbalimbali jijini hapa.

Hata hivyo Mkurugenzi amesema kwa sasa mmiliki wa ghala hilo tayari ameshafikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

Naye Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula wa ZFDA Suleiman, Akida Ramadhan ameta a wito kwa wananchi kuangalia na kuzichunguza kwa makini wakati wanaponunua bidhaa zao iwapo watakugundua kuna hitilafu yeyote wanapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news