Utabiri wa hali ya hewa Desemba 26, 2020 'UPEPO MVUA KUBWA'

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Desemba 26, 2020 unaletwa na mchambuzi Ramadhani Omary kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
ANGALIZO

VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA IRINGA, NJOMBE, LINDI, MTWARA, RUVUMA PAMOJA NA MAENEO YA KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO.

ANGALIZO

VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KILOMITA 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2.0, VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA MTWARA, LINDI, TANGA, DAR ES SALAAM NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA.

Post a Comment

0 Comments