Wafamasia wakumbushwa kuhuisha leseni zao kabla ya mwaka kuisha

Wafamasia nchini wamekumbushwa kuhuisha leseni zao kabla ya tarehe 31 Disemba mwaka huu ili waweze kuendelea kufanya kazi za kitaalam kwa mwaka unaokuja,anaripoti Catherine Sungura (WAMJW) Dodoma.
Msajili wa Baraza la Famasi Bi. Elizabeth Shekilaghe akisisitiza jambo wakati akiongea na Afisa Habari wa Wizara (hayupo pichani) ofisini kwake jijini dodoma ambapo amewakumbusha wafamasia wote nchi kuhuisha leseni zao mwisho ni Desemba 31. (Picha na WAMJW).

Wito huo umetolewa leo na Msajili wa Baraza la Famasi, Bi. Elizabeth Shekalaghe wakati akiongea na afisa habari wa Wizara ya Afya,ofisini kwake jijini Dodoma.

Bi. Eliza amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu Namba 22 cha Sheria ya Famasi sura 311 kinawataka wafamasia kuweza kuhuisha majina yao kwenye rejista kwa utaratibu maalamu.

"Pamoja na baraza la famasi kuwasajili wanataaluma kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya famasi nchini,kifungu kinatutaka kujisajili kila tarehe 31disemba kila mwaka ili kuweza kufanya kazi za kitaalam kwa mwaka unaokuja,"amesisitiza Msajili.

Kwa upande wa uuzaji wa dawa ,Masajili wa baraza hilo Bi.Shekalaghe amesema, tatizo la uuzaji wa dawa kiholela imekua ni tatizo sugu hapa nchini na hivyo mwaka huu Waziri wa Afya ameidhinisha kanuni za uuzaji,usimamizi wa uzaji wa dawa za cheti na hivyo amewataka wanataaluma wa famasi kuhakikisha wanazisoma na kuzielewa kanuni hizo.

"Kama wafamasia na wataalam tukumbuke tuna watu tunawasimamia na kuhakikisha dawa tunazitoa kwa kuzingatia miongozo iliyopo na baraza halitosita kumchukulia hatua yeyote atakayeenda kinyume na kanuni hizo,"ameongeza Bi.Shekalaghe.

Mbali na hayo Bi. Shekalaghe amewataka wananchi kutoa taarifa kwenye baraza hilo pale wasiporidhika na huduma zitolewazo kwa kupiga namba bila malipo 0800110015 ili waweze kutatua changamoto wanazozipata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news