Wahasibu, wakaguzi wa hesabu za Serikali 900 watembelea Mradi wa SGR

Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali Tanzania wamembelea mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kwanza Dar es Salaam mpaka Morogoro wilayani Kilosa mara baada ya kuhitimisha mkutano wao wa mwaka uliofanyika ndani ya mwezi huu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ziara hiyo imeongozwa na meneja mradi wa reli ya kisasa Dar es Salaam- Morogoro na Morogoro - Makutupola, Singida. 
Wahasibuu hao wametumia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Morogoro katika wilaya ya Kilosa wakiwa na lengo la kuona hatua na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa ambao katika mkutano wao wa mwaka mradi wa reli ya kisasa - SGR umekuwa ni ajenda nyeti katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

Aidha, safari hiyo ilianzia katika Stesheni ya Kamata jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, MasanjaKadogosa aliwapokea na kuambatana nao mpaka stesheni ya SGR Soga mkoani Pwani.

Pia alipata nafasi ya kuzungumza na jopo la wahasibu na kuwafafanulia kwa kina namna reli ya kisasa itakavyofungua mianya chanya ya biashara na maendeleo ya uchumi kwa nchi na watanzania kwa ujumla.

“Reli hii itakapokamilika itafungua milango mingi ya kutengeneza uchumi wa watanzania, katika stesheni zetu kuna fursa nyingi za Kibiashara ambazo watanzania wanaweza kuwekeza na kukuza uchumi wa nchi. Katika stesheni zetu tutakuwa na sehemu za maduka, hoteli, na benki wafanyabiashara wakiwekeza watapanua biashara na uchumi utakuwa kwa kasi,"amesema Mkurugenzi Mkuu.

Mara baada ya Mkurugenzi Mkuu kutoa taarifa ya maendeleo ya mradi pamoja na kutambulisha fursa za biashara ziara hiyo iliendelea kuelekea mkoani mkoani Morogoro.

Kupitia usafiri wa treni wahasibu wamejionea maendeleo ya mradi sambamba na kazi mbalimbali za ujenzi zinazoendelea ikiwemo uwekaji wa miundombinu ya umeme, utengenezaji wa tuta pamoja na ujenzi wa madaraja na vivuko

Hata hivyo, wahandisi kutoka Shirika la Reli Tanzania waliendelea kutoa taarifa za maendeleo ya mradi sambamba na kuelezea namna ujenzi wa reli ya kisasa unavyo fanyika hatua kwa hatua. 

Vile vile Wahasibu hao walipata nafasi ya kuuliza maswali kadha wa kadha kuhusu ujenzi wa reli pamoja na taarifa ya fedha zilzotumika katika ujenzi na manunuzi ya malighafi za ujenzi. 

Katika hatua nyingine, Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kwa shauku kubwa walifika mkoani Morogoro Wilaya ya Kilosa ambapo walitembelea na kuona ujenzi wa mahandaki ambayo yatatumika kupitisha treni. 

Wahasibu hao wameshuhudia na wameridhika kuona namna pesa za watanzania zinavyotumika na thamani ya pesa ilivyoendelea kuzingatiwa katika ujenzi wa reli ya kisasa,

Zaidi wametoa pongezi za dhati kwa Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania kwa usimamizi thabiti katika kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ufanisi kulingana na thamani ya fedha.

Naye, Mkurugenzi wa Fedha kutoka Shirika la Reli Tanzania, Bw. Emmanuel Balele ambaye ni mjumbe wa mkutano wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu za Serikali Tanzania, amewashukuru na kuwakaribisha tena wahasibu hao kutembelea mradi wa reli ambao katika mkutano wao ujio wa reli ya kisasa imekuwa ni ajenda kubwa katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na watanzania kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news