Waturuki waonyesha utayari kuwekeza Tanzania

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akielezea juu ya ziara ya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Uturuki katika studio za Radio Uhuru (Uhuru FM) jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiwa na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) na Mamlaka ya Kanda za Kusindika Usafirishaji Tanzania (EPZA) wakiwa tayari kwa kikao kazi. Wadau hao wamekutana kwa pamoja katika ofisi za TIC jijini Dar es Salaam kuwaelezea wawekezaji kuhusu fursa mbalimbali za biashara zilizopo nchini. Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki wakifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa katika Ofisi za TIC jijini Dar es Salaam.Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto), wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, TCCIA, TPSF na SIDO wakisikiliza mada iliyokuwa inahusu fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Kardag kutoka Uturuki ambae pia ni mmoja kati ya wawekezaji akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news