Waziri Mhagama:Wafanyakazi OSHA tekelezeni majukumu yenu kwa weledi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaasa wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi ili kuwa na tija katika kuchangia uchumi wa kati, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wajumbe wa Mkutano wa Baraza ala Wafanyakazi la Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) walipokutana Desemba 17, 2020 Mkoani Morogoro kujadili masuala ya ofisi yao.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wakala hiyo uliofanyika Desemba 17, 2020 mkoani Morogoro kwa kuzingatia ni chombo muhimu kwa watumishi kukutana kujadili masuala muhimu ya taasisi yao na kufanya maamuzi. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) pamoja na wajumbe wa meza kuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Mkutano wa Baraza hilo.

Waziri Mhagama ameeleza ipo haja ya kila mtendaji katika Taasisi hiyo kuona umuhimu wa kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kuzingatia mchango unaotolewa na OSHA katika kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati kwa kuzingatia majukumu yake ya msingi.
“Jitihada za OSHA katika kutekeleza majukumu yake zina mchango mkubwa kuendeleza uchumi wa viwanda na kuboresha mazingira ya biashara na Uwekezaji nchini na ni ishara ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, ya kukuza viwanda,”amesema Waziri Mhagama.

Ameongezea kuwa, kuwe na jitihada za makusudi za kila mfanyakazi kutambua umuhimu wa kubadili mitazamo hasa kiutendaji kwa kuondokana na mazoea na kuendana na kasi ya Awamu hii.

“Hatuna budi kubadilika kifikra na hasa katika utendaji wa kazi zetu za kila siku. Tuepuke kufanya kazi kama tulivyozoea zamani pamoja na ufinyu wa rasilimali fedha uliopo hivyo Menejimenti tunatakiwa kujipanga ipasavyo kusimamia upatikanaji wa haki za wafanyakazi na wafanyakazi kutimiza wajibu wao,”amesisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bi. Khadija Mwenda alieleza jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika ofisi yake ili kuhakikisha wanaendelea kuwa na matokeo chanya ni pamoja na marekebisho ya sheria kuhusiana na tozo na ada, kuondoa urasimu, usimikaji wa mfumo wa tehama, uratibu wa ukaguzi kupitia makao makuu ya taasisi/kampuni na kuongeza uwajibikaji.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda akieleza kuhusu utekelezaji wa majuku wa Ofisi yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa mkutano huo.

“Wakala umeongeza uwajibikaji na kuimarisha mifumo ya usimamizi kwa kuanzisha dawati la kushughulikia kero na malalamiko mbali mbali ya wadau pamoja na kuazishwa kwa utaratibu wa wakaguzi wake kufanya kaguzi kwa timu badala ya mkaguzi mmoja mmoja ambapo itaongeza uwazi katika ukaguzi na hivyo kuongeza ubora na ufanisi katika utoaji huduma na kuondoa usumbufu,”amesema Khadija.
Mwakilishi wa Baraza Kuu Serikalini Bw. Fidelis Gakuba akitoa salamu wakati wa mkutano huo.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Kinondoni Bi. Sarah Rwezaura akitoa salamu wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la OSHA wafuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la OSHA wafuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la OSHA wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano wakati wa Mkutano huo. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Alimemalizia kwa kuitoa hofu jamii kuwa, watatekeleza maelezo ya Waziri pamoja na kuhakikisha wanaondoa urasimu katika utoaji huduma hasa katika yale maeneo yenye viashiria hivyo ikiwemo, muda wa kupata cheti cha Usajili sehemu ya kazi pamoja na kupunguza muda wa kushughulikia kutoka siku 14 hadi siku 1 baada ya mwombaji kukamilisha mahitaji yote ya usajili na kutoa leseni ya Kukidhi matakwa ya Sheria ya Afya Mahali pa Kazi kutoka siku 28 hadi siku 3 baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news