Chelsea kuwapiga bei wachezaji saba

Klabu ya Chelsea inatarajia kuwauza wachezaji wake saba ndani ya mwezi huu ili kuwanasa Declan Rice na Erling Haaland, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Taarifa za awali zimedokeza kuwa Kocha Frank Lampard kwa sasa macho na masikio yake yapo kwa Erling Braut Haaland wa Borussia Dortmund na Declan Rice wa West Ham United.
Kocha wa Chelsea, Frank Lampard. (Picha na football365).

Hatua hiyo inatajwa ni mkakati wa matokeo makubwa ambayo yanatarajiwa kuletwa ndani ya kikosi hicho baada ya muhula wa uhamisho kukamilika. Dhamira yao ikiwa ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2020/2021.

Klabu hiyo inaelezwa kutumia mabilioni ya fedha kujiweka sawa huku wakisajili nyota kadhaa akiwemo kipa Edouard Mendy, Kai Harvertz, Hakim Ziyech,Timo Werner, Xavier Mbuyamba, Malang Sarr, Ben Chilwell na wengine.

Kati ya wachezaji saba ambao Chelsea inatarajiwa kuwaacha ni Marcos Alonso na Antonio Rudiger ambaye ameonekana mara moja katika ligi hadi sasa. Wengine ni Jorginho, Danny Drinkwater, Victor Moses, Andreas Christensen, Ross Barkley ambaye kwa sasa anachezea Everton chini ya kocha Carlo Ancelotti kwa mkopo.

Licha ya Chelesea kumuhitaji Haaland pia anamenyelewa na Manchester City na Manchester United ambao pia wanamsaka kiungo wa Dortmund, Jadon Sancho. 

Haaland anatajwa kuwa miongoni mwa washambuliaji matata katika soka ya bara Ulaya na ameifungia klabu yake jumla ya mabao 17 kutokana na mechi 14 za hadi kufikia sasa katika msimu huu. 

Wakati huo huo, Rice alianza kuhusishwa na Chelsea mwanzoni mwa msimu wa 2018-19 na alikuwa sehemu ya kikosi cha West Ham kilichopokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka Chelsea katika michuano ya la EPL mwezi Disemba 2, mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments