Matusi yamuadhibu mshambuliaji wa Manchester United

Mshambuliaji wa Manchester United, Edison Cavani amesimamishwa kucheza mechi tatu na kutozwa faini ya Euro 100,000 ( zaidi ya sh.milioni 28) ikiwemo kutakiwa kukamilisha mafunzo ya ana kwa ana kuhusu nidhamu, ni kwa kutumia maneno ya kichochezi na matusi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Nyota huyo amelimwa adhabu hiyo kutokana na utovu huo wa nidhanu, baada ya kuandika ujumbe huo kwa Kihispania na kuuchapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii. 

Cavani ambaye ni raia wa Uruguay alikiri kosa lake aliposhtakiwa na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) Desemba 17, 2020 kwa matumizi ya maneno ambayo yalitafsriwa kama kuwavunjia watu heshima.

Nyota huyo aliandika maneo hayo machafu mtandaoni baada ya kufunga bao la ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Novemba 29, 2020. 

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain (PSG) alifuta ujumbe huo wa kichochezi na matusi.

Mbali na kuikosa mechi ya EPL dhidi ya Aston Villa pia kiungo huyo wa zamani wa Palermo na Napoli atakosa mechi ya nusu fainali ya Carabao Cup itakayowakutanisha Manchester United na Manchester City Januari 6, 2021 na mchuano wa raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Watford Januari 9, mwaka huu.

Matumisi ya maneno machafu, kejeli na matusi ni miongoni mwa mambo ambayo yanapigwa marufuku katika sekta mbalimbali ikiwemo michezo ili kuepuka kuwagawa watu na kuzua taharuki. 

Post a Comment

0 Comments