Carlos aokoa jahazi la Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar

Carlos Sténio Fernandes Guimaraes do Carmo, maarufu kama Carlinhos dakika ya 73 imetosha kuipati Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni katilka mtanange mkubwa ambao ulichezwa katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam Februari 20,2021.

Nyota huyo alifunga bao hilo dakika moja tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi akimchambua kipa hodari wa Mtibwa, Abdultwalib Mshery baada ya kupokea krosi nzuri ya winga Mkongo, Tuisila Kisinda.

Awali Mtibwa Sugar walifanikiwa kuwabana Yanga tangu mwanzo wa mchezo na kuwaweka roho juu mashabiki wa Yanga SC ambao timu yao imetoka kutoa sare tatu mfukulizo katika Ligi Kuu.

Sare hizo ni 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City zote ugenini Sumbawanga na Mbeya na 3-3 nyumbani dhidi ya Kagera Sugar.

Aidha, kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha alama 49 baada ya kucheza mechi 21 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa alama saba zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu, KMC imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, wakati Ihefu SC imeichapa 3-2 Mwadui Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news