Changamoto za kiutendaji kwa wadau wa madini zitatuliwe mara moja-Prof. Manya

Naibu Waziri wa Madini,Prof. Shukrani Manya amesema changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Wadau wa Madini wakati wa kujadili mada za siku ya kwanza ni za kiutendaji hivyo zitatuliwe mara moja, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dar es Salaam).

Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya akitoa maelekezo ya Serikali wakati akihairisha Mkutano kwa siku ya kwanza unaoendelea jijini Dar es Salaam. Mada mbili zimejadiliwa ikiwa ni kuhusu madini ya viwandani na ile iliyohusu madini ya vito.

Amesema suala la kutafsiri lugha wanapotoa taarifa mara baada ya wachimbaji wadogo kuwasilisha sample zao kwa ajili ya vipimo lianze kufanyiwa kazi na taarifa hizo ziandikwe kwa lugha ya kiswahili lugha rafiki kwa wadau wetu.

Aidha, Naibu Waziri Prof. Manya ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti (GST) kuhakikisha vifupisho vinavyotumika katika miongozo mbalimbali ya wachimbaji wadogo iwe ni ile ambayo wadau wa Madini wanaweza kuelewa.

Amekiri kuwa Mikutano hii inatuleta pamoja ili kutuonesha fursa ambazo kila mmoja ataweza kuona fursa na kunufaika.

Ameyasema hayo wakati akiahirisha Mkutano wa Kimataifa wa Madini kwa siku ya kwanza unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 21 Februari, 2021.

Mjiolojia Marovoku Msechu, akiwasilisha mada iliyohusu Madini ya Viwandani akiwa ni mtoq mada wa kwanza kwa siku ya kwanza ya Mkutano wa Kimataifa wa Madini utakaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Viongozi waandamizi wa Wizara, Doto Biteko kushoto na Naibu Waziri wake Prof. Shukran Manya wakifuatilia mada wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Madini unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Saalam.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wa madini Mkoani Arusha, Jeremiah Simon Kituyo akichangia mada wakati wa majadiliano ya mada ya madini ya vito iliyowasilishwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Yahya Samamba leo tarehe 21 Februari, 2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akifuatilia mada majadiliano yakiendelea wakati wa siku ya kwanza Mkutano wa Kimataifa wa Madini ulionza tarehe 21 Februari, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news