Dkt.Ndumbaro:Watumishi tulinde afya zetu ili tuwahudumie wananchi

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro, amewataka Watumishi wa Umma nchini kulinda afya zao ili waweze kuwahudumia vema wananchi wanaofuata huduma mbalimbali katika taasisi zao, anaripoti James Mwanamyoto (OR-Utumishi) Dodoma.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo mapema leo wakati akizungumza na Watumishi wa ofisi yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Dkt. Ndumbaro amesema, ili Watumishi wa Umma waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hawana budi kulinda afya zao ikizingatiwa kuwa wakati wa utoaji huduma wanakutana na watu ambao baadhi yao wanaweza kuwa na changamoto mbalimbali za kiafya.

Ili kuhakikisha taifa linakuwa na rasilimaliwatu yenye tija, Dkt. Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara na kupata tiba mapema iwezekanavyo pindi wanapohisi kukabiliwa na changamoto yoyote ya kiafya.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa ofisi yake leo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na watumishi hao kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

 Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Sanjali na hilo, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi wa Umma kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya kwa lengo la kuendelea kutoa mchango katika ujenzi wa taifa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro amekuwa na utaratibu wa kukutana na Watumishi wa Umma katika maeneo mbalimbali nchini kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news