🔴LIVE:SIMBA SC Vs AL AHLY 'Total War, Point of No Return'

 Leo Februari 23, 2020 dimba la Benjamin Mkapa lillopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wekundu wa Msimbazi, Simba SC wanamenyana na mabingwa wa soka wa Afrika, Al Ahly ambao ni wageni wa Simba, ambao kwa sasa wako moto baada ya kushinda mechi yake ya kwanza ugenini dhidi ya timu ngumu ya AS Vita. 

Simba SC wameipa mechi hiyo jina la Total War, Point of No Return (vita kamili, nyuma mwiko) kuonyesha umuhimu wa ushindi leo baada ya kampeni ya kwanza ya War in Dar (WIDA) kushuhudia vigogo hao wa soka nchini wakiisambaratisha Platnum FC ya Zimbabwe kwa mabao 4-0 na kugeuza ushindi wa kwanza wa bao 1-0 jijini Harare na hivyo kufuzu kucheza hatua ya makundi.

Aidha, huku kila timu ikiwa na alama tatu mkononi, mchezo wa leo wa raundi ya pili ya Kundi A unatarajiwa kuwa wa kufa na kupona kama vyombo vya habari vya Misri vinavyouelezea. 

MATOKEO

Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.  

Mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 31, limetoka kwa kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kwa shuti la umbali wa mita 20 baada ya kuwahadaa viungo wa Ahly  Aliou Dieng, raia wa Mali na Mmisri Akram Tawfik kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama.

Kwa ushindi huo, Simba inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili kufuatia ushindi wa ugenini wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AS Vita mjini Kinshasa Febaruari 12, mwaka huu.

 Baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, E l Merreikh leo Uwanja wa Al-Hilal Jijini Omdurman, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inakaa nafasi ya pili ikilingana pointi na Al Ahly. 

Mechi ijayo SImba SC watakuwa wageni wa El Merreikh nchini Sudan na Al Ahly watakuwa wenyeji wa AS Vita Jijini Cairo Machi 5, mwaka huu.

Squads & Team News

Position Simba SC squad
Goalkeepers Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim Juma.
Defenders Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Peter Muduhwa, Kennedy Juma, Gadiel Michael, Mohamed Hussein.
Midfielders Tadeo Lwanga, Jonas Mkude, Larry Bwalya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Francis Kahata, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Bernard Morrison.
Forwards Meddie Kagere, Athumani Miraji, Chris Mugalu, and Junior Lokosa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news