Mabalozi wa Tanzania popote walipo watakiwa kuipa Diplomasia ya Uchumi kipaumbele

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kuongeza jitihada za kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi inaleta tija iliyokusudiwa, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dar es Salaam).

Balozi Ibuge ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe, Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbenna.

Balozi Ibuge katika mazungumzo yake na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Prof. Mbennah amemtaka kuhakikisha kuwa anafanya kazi kwa weledi katika kuimarisha uhusiano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zimbabwe pamoja na kukuza diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali.

“Balozi nakusihi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kufanikisha azma na malengo ya Serikali katika kuhakikisha tunaimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia na Zimbabwe lakini pia kukuza diplomasia ya Uchumi kati yetu na Zimbabwe,” Amesema Balozi Ibuge.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Eva Ngitu Msaidizi wa Katibu Mkuu.

Kwa upande wake, Balozi Prof. Mbennah amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa uhusiano wa Jamhuri ya Muungano na Tanzania na Zimbabwe ni mzuri na imara.

Katika tukio jingine, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili umuhimu wa kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika ipasavyo na uhusiano mzuri wa kidiplomasia ilionao na Marekani.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi

Katika kuhakikisha hilo, Balozi Ibuge alimsisitiza Balozi Masilingi kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa manufaa ya Taifa.

Nae balozi Masilingi amemhakikishia Katibu Mkuu kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani unaendelea kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa kasi inayotakiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news