Namungo FC yaichapa De Agosto mabao 6-2

Namungo FC imeibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya wapinzani wao Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Afrika, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ushindi huo mnono wameupata leo Februari 21, 2021 katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi ndani ya Manispaa ya Temeke,Dar es Salaam.

Vijana wa Lindi, Namungo FC walikuwa wa kwanza kufungwa bao kabla ya kusawazisha bao hilo na kupata mabao mengine na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho Namungo FC aliibuka na ushindi wa mabao 6-2.

Magoli ya Namungo yamefungwa na Hashim Manyanya (32’), Sixtus Sabilo (38’, 59’), Reliants Lusajo (55’), Erick Kwizera 66’ na Stephen Sey dakika ya 72.

Mechi ya marudiano itapigwa ndani ya saa 72 zijazo, na Namungo itahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 4-0 ili kungia hatua ya makundi ya michuano hii ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.


No comments

Powered by Blogger.