Ndejembi akemea waajiri wanaowabadilisha vyeo vya kimuundo kinyume na taratibu maafisa tarafa na watendaji kata walioajiriwa 2018

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Waajiri kutowabadilishia vyeo vya kimuundo Maafisa Tarafa na Watendaji Kata walioajiriwa mwaka 2018 wakiwa na taaluma mbalimbali kwa lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliostaafu na walioondolewa baada ya kubainika kuwa na vyeti vya kughushi, anaripoti James K.Mwanamyoto (OR-Utumishi) Iringa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani Iringa kwenye Ukumbi wa Manispaa wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi hao.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo Mkoani Iringa wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali mkoani humo.

Mhe. Ndejembi amesema, wapo baadhi ya Waajiri wamewabadilishia watumishi hao vyeo vya kimuundo bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye mwenye mamlaka ikizingatiwa kuwa alishatoa maelekezo ya kutowabadilishia kada wala kuwahamisha vituo vya kazi mpaka watakapotimiza miaka mitano.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani Iringa wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akizungumza nao kwenye Ukumbi wa Manispaa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi hao.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda akiwasilisha changamoto za kiutumishi zinazowakabili watumishi mkoani Iringa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.

"Watumishi hao wakati wa kuajiriwa, walisaini mikataba ya kutumikia vyeo vyao bila kubadilisha wala kuhama mpaka watakapotimiza miaka mitano, hivyo Waajiri kama mna upungufu wa Watumishi ambao wana sifa walizonazo watumishi hao, muombe kibali kwa Katibu Mkuu Utumishi ili mpatiwe watumishi mbadala." Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema changamoto ya Watumishi wa Umma kukaimu nafasi za uongozi kwa muda mrefu inatokana na baadhi ya waajiri kuwakaimisha Watumishi nafasi mbalimbali bila kuwa na kibali cha Katibu Mkuu Utumishi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akijibu hoja za kiutumishi zilizowasilishwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Iringa yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma mkoani humo.

Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, asilimia zaidi ya 60 ya wanaokaimu hawana sifa za kutumikia vyeo walivyokaimishwa, hivyo wanapoteza sifa za kupata kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na stahiki husika.

Ametoa wito kwa Waajiri kuwaombea vibali kwa wakati kwa Katibu Mkuu Utumishi watumishi ambao wana sifa za kukaimu ili waweze kupata uhalali wa kutumikia vyeo walivyokasimiwa na kupata stahiki husika na kuongeza kuwa, hivi sasa ofisi yake inatoa vibali vya kukaimu kwa wakati ndani ya wiki tatu.

Mhe. Ndejembi amefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Wakuu wa Idara na Taasisi za Umma zilizopo mkoani humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news