Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi wa maofisa wadhamini, majaji

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa maofisa wadhamini, Pemba katika Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, alieleza kwamba uteuzi huo umeanza leo Februari 4, 2021.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais Dkt.Mwinyi chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu cha 12 cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2011 aliwateua;

Dkt.Fadhil Hassan Abdallah kuwa Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Halima Khamis Ali kuwa Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Abdulwahab Said Abubakar kuwa Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Wengine ni Thabit Othman Abdalla anayekuwa Ofisa Mdhamini Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Ahmed Abubakar Mohamed ambaye anakuwa Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Ali Salim Matta anakuwa Ofisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Ibarahim Saleh Juma Ofisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Zuhura Mgeni Othman anakuwa Ofisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Mhandisi Suleiman Hamad Omar anakuwa Ofisa Mdhamini Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Yakoub Mohamed Shoka, Ofisa Mdhanini Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Bakari Ali Bakari Ofisa Mdhamini Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi na Dkt. Salum Mohamed Hamza Ofisa Mdhamini Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.

Kwa upande wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyeteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini ni Salum Ubwa Nassor, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda aliyeteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini ni Ali Suleiman Abeid na Mohamed Nassor Salim anakuwa Ofisa Mdhanini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.


No comments

Powered by Blogger.