Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ameivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuanzia leo tarehe 24 Februari,2021, anaripoti Mwandishi Diramakini (Dar es Salaam).

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa taarifa hiyo jioni ya leo kwenye Ofisi ndogo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Magogoni Jijini Dar Es Salaam.
 
“Hii ni kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 84 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) sura ya 288,”amesema Waziri Mhe.Jafo.

Post a Comment

0 Comments