Serikali yaagiza Somo la Michezo kufundishwa shule zote nchini

Serikali imewaagiza wakuu wa shule zote za msingi na sekondari nchini kuhakikisha somo la michezo linafundishwa ipasavyo ili kuwaandaa vijana vyema katika michezo mbalimbali, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza jambo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na sekondari,Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.

Azimio hilo limefikiwa Februari 8, 2021 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kilichoandaliwa na Wizara ya Habari ambacho kilijadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na sekondari.

“Nawaagiza walimu wakuu wa shule zote nchini, kusimamia vyema vipindi vya michezo kwa kuhakikisha somo hilo linafundishwa na limeruhusiwa kuwepo kwenye mitaala na katika muda sahihi,wanafunzi washiriki vyema vipindi vya michezo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akikazia jambo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na sekondari, Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.

Waziri wa Habari.Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akieleza mipango mbalimbali ya kuendeleza michezo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na sekondari, Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas mara baada ya kumaliza kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na Sekondari, Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Yusuph Singo(kushoto mwenye miwani) akiwasilisha hoja za wizara yake katika kuboresha michezo katika shule za msingi na Sekondari Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.

"Na sisi upande wa Serikali tutasimamia vyema ajenda hiyo na tutahakikisha maafisa elimu mkoa na wilaya wanafuatilia michezo katika maeneo yao,”amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo.

Mhe.Jafo ameeleza kuwa ili kuleta ufanisi katika michezo, ni wajibu kwa halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za michezo na kuwaagiza wakurugenzi katika halmashauri hizo kusimamia vyema miundombinu ya michezo na kuhakikisha maeneo ya michezo hayavamiwi.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof. Joyce Ndalichako amesema, wizara yake inakamilisha uandaaji wa michepuo ya masomo ya michezo na kuhuisha mitaala iliyopo ili somo hilo lilete tija kwa wanafunzi ambao baadhi wameanza kulifanyia mitihani katika kidato cha nne na sasa taratibu zinakamilishwa masomo hayo yaendelee hadi kidato cha tano na sita hali itakayosaidia nchi kupatawataalamu wengi zaidi.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amezishukuru wizara hizo kwa kuzingatiadhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli ni kuleta uhai katika timu za Taifa ambao unatokana na kuwepo kwa vipaji vinavyozalishwa kuanzia shule za msingi na sekondari.

Aidha, kikao pia kimeazimia kuhuisha ufanisi wa mashindano ya michezo ya sekondari na shule za msingi ikiwemo kuunda Kamati mpya ya Kitaifa na kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya shughuli za michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA) naUmoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

No comments

Powered by Blogger.