Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 11th, 2021


 UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:

TAREHE: 11/02/2021.

Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara Ruvuma pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, Mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

.........

Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Manyara, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga, Morogoro (Kaskazini) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

........

Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.......

ANGALIZO

1. VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA LINDI, MTWARA, NJOMBE, RUVUMA, IRINGA PAMOJA NA KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO.


2. VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WOTE WA PWANI KATIKA MIKOA YA LINDI, MTWARA, DAR-ES-SALAAM, TANGA NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA), PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA.

..........

VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI                 Kiwango cha juu         Kiwango cha chini 

                       cha joto                      cha joto

ARUSHA         26°C                           17°C 

D'SALAAM      32°C                           25°C 

DODOMA       28°C                           19°C

KIGOMA         27°C                            21°C 

MBEYA            21°C                           16°C 

IRINGA            23°C                           16°C 

NJOMBE         19°C                            11°C 

MWANZA       29°C                            21°C 

TABORA          26°C                           19°C 

TANGA            32°C                           25°C 

ZANZIBAR       32°C                           25°C

..........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.

Matarajio kwa siku ya Jumamosi tarehe 13/02/2021: Mabadiliko kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 11/02/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news