Waziri Jafo asisitiza kampeni ya kuorodhesha nyumba nchini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo asisitiza umuhimu wa kufanya kampeni ya kuorodhesha nyumba zote nchini kwa lengo la kukusanya mapato,anaripoti Angela Msimbira (OR-TAMISEMI).
Ameyasema hayo leo kwenye Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wakati akikagua miradi ya Maendeleo Mkoani Morogoro.
 
Amesema kuwa kampenni hiyo itaanza tarehe 15 hadi 28 Februari 2021 na kuwaagiza Watendaji wote wa Serikali za Mitaa na vijiji kuanza kupita nyumba kwa nyumba kuorodhesha majengo yote kuachilia majengo ya Tasisi za dini ili kuhakikisha Serikali inapata kodi kwa ajili ya mstakabali wa Taifa.

Aidha, Waziri Jafo ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji ili kuwawezesha wawekezaji kuwekeza nchini kwa kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha maeneo yanatengwa.

No comments

Powered by Blogger.