WAZIRI KALEMANI: KUUNGANISHA UMEME NI ULIPO TUPO

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amesema kuwa, kazi ya kuunganisha umeme kwa wananchi kwa sasa ni, "popote ulipo tutakuletea umeme", anaripoti Robert Kalokola (Geita).

Dkt.Kalemani ameyasema hayo Februari 17,2021 alipokuwa akiongea na wananchi wa kata za Bwongela na Muganza wilayani Chato Mkoa wa Geita alipokwenda kukagua kazi ya usambazaji umeme inayoendelea katika vitongoji vya kata hizo.
Waziri Kalemani akiwasha umeme katika Kanisa la Waadiventista Wasabato katika Kijiji cha Mkombozi Mkoa wa Geita. (Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).

"Haijalishi nyumba yako ni ya nyasi, udondo au ya bati, sisi popote utakapo kuwepo tutakutundikia umeme,"amesema Dkt. Kalemani.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani katika Kijiji cha Bwongela Wilaya ya Chato mkoa wa Geita.(Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).

Aidha amewataka wananchi wote ambao hawajafanya hawajatandaza mfumo wa nyaya kwenye nyumba zao (wiring) wafanye hivyo ili waweze kuwekewa umeme Mara moja.

Waziri Kalemani ameelekeza TANESCO nchi nzima kuwafungia umeme wateja waliokwisha kulipia umeme ndani ya Siku 30 na kununua pikipiki ili ziweze kutumiwa na Saveya wa Shirika hilo ili kuepuka usumbufu kwa watu kukaa muda mrefu bila kufanyiwa tathmini ya gharama wanazotakiwa kulipa.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani akiongea na wananchi wa kijiji cha mkombozi,kata ya muganza,wilayani Chato-Geita. (Picha na Robert Kalokola/ Diramakini).

"Na hili ni agizo kwa TANESCO nchi nzima muwanunulie masaveya bodaboda, waweze kufanya kazi kwa kasi tunayoitaka," amesema Dkt.Kalemani.

Vile vile amewataka wananchi ambao tayari wameshapata umeme kuutumia umeme kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji mazao na mashine za kusaga na kukoboa ili matunda ya umeme yaonekane katika vipato vyao.

No comments

Powered by Blogger.